.

.

.

.

Wednesday, 21 June 2017

HII NDIO NJIA RAHISI AMBAYO UNAWEZA KUITUMIA KUZALISHA KUKU CHOTARA

HII NDIO NJIA RAHISI AMBAYO UNAWEZA KUITUMIA KUZALISHA KUKU CHOTARA



Leo tutaangalia kuhusu ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa kutumia njia rahisi. Na jinsi gani unaweza kuzalisha kuku chotara. Kuku chotara ni mchanganyiko wa kuku wa kienyeji na kisasa. Kabla hatujangalia hatua muhimu za kuzalisha kuku chotara, tutaangalia faida za kuku chotara kwa mwekezaji/mjasiriamali.

Faida za kuku chotara kwa mfugaji na mlaji
Ukuaji mzuri 
Nyama  yake ina ladha nzuri na laini
n.k

Hawa ni kati ya kuku chotara ambao ninafuga

HATUA MUHIMU KATIKA UZALISHAJI WA KUKU CHOTARA

Hatua ya kwanza, andaa banda lako ambalo linafaa kwa matumizi ya ufugaji wa kuku, banda la kuku linatakiwa liwe  lina pitisha hewa ya kutosha na kama unataka kufahamu kwa undani kuhusu maandalizi muhimu ya banda lako. Makala hiyo itakuja kupitia blog yako ya uwekezaji na mtanzania.

Hatua ya pil,i andaa kuku wa kienyeji matetea (majike) na jogoo la kisasa aina ya kocks au aina yoyote ile ambayo inafaa, wachanganye kuku wa kienyeji na jogoo la kisasa katika banda moja ili uweze kupata mayayi yenye mchanganyiko wa kuku wa kienyeji na kisasa. Kumbuka jogoo mmoja (1)anatakiwa kuwa na matetea kumi na tano (15) au matetea yasizidi kumi na tano.

Hatua ya tatu kutotolesha mayayi ambayo umeyapata kutokana na mchanganyiko wako, unaweza kutumia mashine za kutotolesha mayayi au unaweza kuwatumia matetea yako ya kuku wa kienyeji kuatamia mayayi yako.

Hatua ya nne baada ya siku ishirini na moja (21), vifaranga vyako vitakuwa tayari kwa kutumia matetea ya kuku wa kienyeji au mashine ya kutotolesha vifaranga kwa ajilia ya matunzo mpaka wakiwa wakubwa. Vifaranga vikishakuwa tayari chanjo muhimu wanahitaji ili kuzuia vifo na mripuko wa magonjwa. Vifaranga kwa muda wa wiki tatu hadi nne wanahitaji joto la kutosha, kwa ajili ya ukuaji afya njema.

Chanjo na dawa muhimu kwa vifaranga mpaka wakiwa wakubwa
Siku 2-6 Pullorum Trisulmycine,Trimazine 30%au Cotrim+Vitalyte,Amin’total au Broiler booster maji
Siku ya 7 Mdondo(newcastle) Newcastle vaccine(Lasota maji
Siku 14 Gumboro Gumboro (Bursine vaccine-IBD) maji
Siku 16-20 Coccidiosis Trisulmycine/Trimazine/Esb3 30%+Dawa yoyote ya Vitamin maji
Siku 21 mdondo(newcastle) Newcastle vaccine(Lasota) maji
Siku 28 Gumboro Gumboro (Bursine vaccine-IBD) maji
Wiki ya 6-8 Ndui Fowl pox vaccine sindano kwenye bawa
Wiki ya 13 minyoo Pipperazine cirtrate+Dawa yoyote ya vitamin maji
Wiki ya 10 hadi ya 15 ukataji midomo Dawa ya vitamin itumike baada ya zoezi maji
 
KUMBUKA
Dawa ya minyoo na chanjo ya kideli kila baada ya miezi mitatu
Share:

HII NDIO BIASHARA UNAYOWEZA FANYA KWA MTAJI MDOGO NA KUTENGENZA PESA?

HII NDIO BIASHARA UNAYOWEZA FANYA KWA MTAJI MDOGO NA KUTENGENZA PESA?



HII NDIO BIASHARA UNAYOWEZA FANYA KWA MTAJI MDOGO NA KUTENGENZA PESA?


Tatizo la ajira limeendea kuwa kikwazo kikubwa cha wahitimu wengi wanaomaliza masomo yao katika ngazi mbalimbali hapa nchini na hata kwa wale ambao hakufanikiwa kuendelea na masomo. Huku sekta ambayo inatoa ajira nyingi kwa wahitimu ni sekta binafsi. JE WE KIJANA UNAKUBALIANA NA TATIZO LA KUKOSA AJIRA HUKU UKISUBIRI SERIKALI?
Suluhisho la tatizo lako liko hapa ndugu, unaweza kujiari kwa mtaji mdogo na ukatengeneza pesa. Nadhani utajiuliza ni biashara gani au ni shughli ipi ambayo inaweza kukuingizia kipato kwa mtaji mdogo. KILIMO CHA UYOGA kati ya biashara ambayo hazihitaji mtaji mkubwani kilimo ambacho hakihitaji mtaji mkubwa sana, kwa wewe kijana ambaye una lengo la kutengeneza pesa hili ni kati ya suluhisho linalokufaha. Bei ya kilo ya Uyoga ni kuanzia Shilingi 6,000 mpaka 12,000 kwa kilo, bei zina tofautia kutokana na maeneo
                                                 
HISTORIA FUPI KUHUSU KILIMO CHA UYOGA HAPA TANZANIA
Miaka ya karibuni, utaalamu wa kuotesha uyoga umeanza hapa Tanzania baada ya watu kutilia maanani lishe bora ya protini na manufaa mengine ya zao hilo. Kwa kuwa uyoga upo wa aina mbalimbali, usitawishaji wake hutofautiana katika mahitaji yake, ikiwa ni pamoja na hali ya hewa, malighafi za kuoteshea, urahisi wa teknologia ya kuotesha katika mazingira ya Tanzania na soko lake kwa wananchi na katika hotel. Hata hivyo ni wananchi wachache tu wanaojua kilimo cha uyoga.

MAHITAJI KATIKA KILIMO CHA UYOGA

Kabla ya kuanza kuzalisha uyoga inabidi kuwa na chumba chenye paa ambalo litazuia jua, mvua, na vumbi. Chumba hiki kinatakiwa kiwe na sakafu inayohifadhi unyevunyevu pamoja na sehemu ya giza ambayo ni muhimu kwa kuotesha utando wa uyoga. Mkulima wa kawaida anaweza kutumia kasha kama sehemu ya giza.

Mbegu za uyoga huzalishwa kwenye maabara zenye vifaa vinavyowezesha kuotesha mbegu hizo bila kuchafuliwa au kuchanganyika na vimelea kama bakteria, ukungu au jamii nyingine za uyoga ambazo haziliwi. 










 Hapa Tanzania hivi sasa maabara hizo zipo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kituo cha utafiti wa kilimo-Uyole na taasisi ya utafiti wa kilimo cha bustani- Tengeru (HORTI – Tengeru, Arusha). Hata kwenye maduka ya kilimo na mifugo.

Mahitaji mengine
1. Pipa
2. Majani ya migomba
3. Maranda 
4. Visado au lailoni
 

Somo hili la kilimo cha uyoga litakuja wiki ijayo kupitia blog yako UWEKEZAJI NA MTANZINIA

Share:

JINSI YA KUANDAA UYOGA

jinsi ya kuandaa mbegu ya uyoga
              
1.       Unatakiwa kuwa na chumba maalumu kisichopitisha mwanga
2.      Unatakiwa kuwa na presure cooker au jiko maalumu lenye moto mkali.
3.      Vyombo vya kuwekea mbegu kama vile glass, maji salama, ungaunga wa viazi vitamu, uteute unaotokana na mchemsho wa viazi vitamu pamoja na kibakuli kidogo chenye mfuniko.
4.      Kipande cha uyoga ambacho kitachanganywa na maji salama, ungaunga wa viazi vitamu, uteute unaotokana na mchemsho wa viazi vitamu,  kwa ajili ya kutengeneza fangasi ambao watatumika kutengeneza mbegu ya uyoga.
5.      Baada ya  kuchanganya  mchangnyiko huo, chemsha mchanganyiko huo kwenye presha cooker au jiko la moto mkali.
6.      Ipua na weka mchanganyiko huo kwenye vibakuli vidogo vinne vyenye mfuniko [4]
7.      Acha  upoe kwa dakika kumi na tano.
8.     Chukua vipande vya uyoga weka kwenye mchanganyiko  uliouweka kwenye bakuli ndogo yenye mfuniko  halafu funika na hifadhi sehemu yenye joto ili kukuza fangasi kwa muda wa siku kumi au kumi na tano.
9.      Baaada ya siku kumi na tano fangasi zitakuwa tayari kwa ajili ya kuendelea kuandaa mbegu ya uyoga.
10.  Hifadhi fangasi hao kwenye friji ili wasiendelee kukua.

Baada ya kuandaa fangasi hatua inayofuata ni;


1.        Andaa mtama kilo hamsini [ kg 50]
2.      Chemsha mtama  kwenye jiko lolote mpaka uive kwa kupasukapasuka
3.      Ipua na chuja maji
4.      Baada ya kuchuja weka mtama wako kwenye chupa au kopo lenye mfuniko,weka katika chupa nyingi  kadiri uwezavyo.
5.       Weka kwenye preasure cooker au jiko lenye moto mkali kwa muda wa saa moja
6.      Ipua na acha upoe
7.      Baada ya kupoa chukua fangasi katakata vipande vipande na kila  kipande weka kwenye kopo au chupa yenye mtama.
8.     Funika kwa muda wa siku kumi na tano mbegu itakuwa imekomaa na tayari kwa kupandwa katika shamba uliloliandaa..  
Aina ya mbegu tuliyoiandaa hapa ni mamama/ oista mashroom.. uyoga zao linalotumika kukuza uchumi kwa wakulima kwani linahitajika sana mahotelini kwa ajili ya supu. lakini uyoga huo pia unatumika majumbani kwa mlo ambao una lishe bora kwa familia.

NB; mahitaji yote unaweza kuyatengeneza ukiwa nyumbani au unaweza kuvipata kwa  kununua kwenye maduka kwa kutumia majina yafuatayo;
-           Agger- ungaunga wa viazi vitamu
-          Distil water-maji salama
-          Bikker –glass
-          Maltexxtract-uteute unaotokana na mchemsho wa viazi vitamu
-          Pret dish-kibakuli kidogo chenye mfuniko.
Share:

UFUGAJI NYUKI KIBIASHARA

Ufugaji Nyuki

Kwa kawaida makundi ya nyuki katika nchi ya Tanzania na baadhi ya nchi zinazolingana kwa tabia za nchi, makundi ya nyuki huanza kutafuta sehemu salama na yenye chakula kwa wingi kuanzia mwezi wa kumi katika mwaka mpaka mwezi wa nne kwa mwaka unaofuata.Kipindi hiki huwa na makundi mengi yanayozunguka hapa na pale kutafuta nyumba ambayo itawafaa kwa ajili ya makazi yao na kwa ajili ya kuhifadhia chakula.

Hiki ndio huwa kipindi muafaka sana kwa wafugaji kuanza kutega mizinga ambayo imeshaandaliwa kwa ajili ya kufugia nyuki.Kwa kuwa makundi mengi huwa yanatafuta sehemu za makazi hivyo ni rahisi sana kuyakama na kuyahifadhi makundi hayo kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya nyuki.

Kutokana na hilo, mfugaji anapaswa kuanza kuandaa sehemu ya kufugiua nyuki na mizinga yake mapema zaidi kabla ya msimu huo kufika ili asiweze kukosa makundi ya nyuki.Unashauriwa kuanza kuandaa mazingira ya kufugia nyuki na mizinga angalau mwezi mmoja kabla kwa kusafisha, kukarabati au kutengeneza kile unachokihitaji.


VIFAA VINAVYOPASWA KUANDALIWA.
Kabla ya kuanza kufuga nyuki kuna vifaa ambavyo mfugaji wanyukiu anapaswa kuanza kuviandaa mapema kabla ya msimu wa ufugaji wa nyuki kufika.Vifaa hivyo ni kama vifuatavyo:-

UJENZI WA MABANDA YA KUFUGIA NYUKI.
Eneo ambalo kuna wanyama wa aina mbalimbali ambao wanaweza kufanya uharibifu mbalimbali wa mizinga pindi ikiwa na nyuki na kusababisha uharibifu wa mizinga, kuua nyuki au hata mnyama mwenyewe kufa kutokana na kudungwa na nyuki.Hivyo ujenzi wa mabanda ya kufugia nyuki ni vyema ukafanyika.

DHAMIRA YA UJENZI WA MABANDA YA KUFUGIA NYUKI.
Mabanda hayo ya kufugia nyuki yanaweza kuwa ya udongo, tofali au ya miti pekee pande zote, milango pamoja na kuezekwa kwa nyasi.
Kuna sababu mbalimbali ambazo zinasababisha mfugaji nyuki kuweza kujenga mabanda ya kufugia nyuki, miongoni mwa sababu hizo ni:-
1.      Kukinga mizinga na jua na mvua.
Hii ni sababu moja wapo ambayo inasababisha mfugaji wa nyuki kuamua kujenga mabanda ya kufugia nyuki, mzinga unapokuwa kwenye kivuli huusaidia mzinga kuweza kudumu kwa kipindi kirefu, pia kivuli husaidia nyuki kufanya kazi zao kwa juhudi.Iwapo mzinga utakuwa upo kwenye jua nyuki hutumia muda mwingi kupunguza joto la ndani ya mzinga badala kutumia muda huo kwa ajili ya kutafuta chakula.

Nyuki wanapoona jua ni kali zaidi na kusababisha joto kali ndani ya mzinga huamua kuhama katika mzinga huo na kwenda kutafuta makazi sehemu nyingine.Hivyo nio vyema mzinga ukakaa kwenye kivuli na sehemu isiyoweza kunyeshewa na mvua.

Pia mvua inaponyeshea mzinga husababisha mbao kuweza kuoza ndani ya muda mfupi, hivyo kwa kujengea banda la kufugia nyuki huweza kuukinga mzinga wako dhidi ya mvua ambayo inasababisha kuozesha mbao za mzinga wako.

2.      Kukinga na wanyama waharibifu
Mabanda haya ya kufugia nyuki husaidia sana kwa wanyama waharibifu wa mizinga kushindwa kuifikia mizinga lakini pia husaidia sana kupunguza mashambulizi ya nyuki kwa viumbe wengine.Mizinga huwekwa ndani ya banda na banda kufungwa milango.

3.      Ulinzi na ukaguaji
Ujenzi wa mabanda ya kufugia nyuki husaidia sana kuiweka mizinga yako sehemu salama dhidi ya wezi wa mizinga au asali lakini pia husaidia sana wakati wa uangalizi wa mzinga.Mizinga inapokuwa pamoja uangalizi wa mizinga hiyo huwa ni rahisi sana na pia huweza kusaidia kipindi cha uvunaji na uwekaji wa kumbukumbu za kila mara.

Pembeni ya banda hilo sehemu ambazo mizinga inawekwa huwekwa matundu maalumu ya kutoka na kuingia nyuki kwa ajili ya kujitafutia chakula chao.

MIZINGA YA KUFUGIA NYUKI.
Mizinga ya kufugia nyuki inapaswa kuandaliwa mapema kabla ya msimu wa kukamata makundi ya nyuki haujafika.Mizinga inayopaswa kuandaliwa ni kama ifuatayo:-

1.      Mzinga wa kibiashara
Huu ni mzinga wa kisasa unaotumika kwa wafugaji wa nyuki hasa wale wanaotaka kuvuna asali kwa wingi kwa ajili ya kuuza.Mzinga huu huweza kuzalisha asali kwa wingi kadri misimu ya uvunaji inavyoongezeka mwaka hadi mwaka.
Mzinga huu una sehemu kuu tatu kama zifuatazo:-
a.      Box la kuzalishia watoto wa nyuki
Ni box ambalo kwa kawaida huwa la kwanza kwa upande wa chini.box hili ndilo ambalo huwa na mlandfo wa nyuki kuingia na kutoka pindi wanapokwenda na kutoka kwenye utafutaji wa chakula.Box hili hutumika na malikia wa nyuki kwa kutagia mayai pamoja na kulelea watoto ambao husubiri kuanguliwa na kuwa nyuki kamili.
Pia box hili hutumika kwa ajili ya nyuki kuhifadhia chakula chao kwa ajili ya msimu wa kiangazi, msimu ambao huwa hauna maua yenye chakula cha nyuki cha kutosha,Hivyo mfugaji hapaswi kuvuna asali anayoikuta katika brood box, kwa kuvuna asali unayoikuta katika brood box husababisha kundi lako kuhama kwa kukosa chakula.
Kwa kawaida matumizi ya mzinga huu huanza kuvuna asali baada ya wastani wa misimu miwili mikubwa yaani sawa na miaka miwili.Na mara baada ya kipindi hicho kipita mfugaji huweza kuanza kuvuna kwa vipindi tofauti tofauti vya mwaka na kuendelea.
b.      Kitenga malikia
Hiki ni kifaa kama nyavu ambacho huwekwa kati ya brood box na super box, wavu huu huweza kumzuia malikia asiweze kupanda katika super box kwa lengo la kutaga mayai.matundu ya waya huu ni madogo kulingana na umbile la nyuki watenda kazi peke yao.Hivyo malikia na madume ya nyuki hayawezi kupanda kuelekea kwenye super box.

c.       Box la kuhifadhia asali
Hili ni box ambalo huwekwa juu mara tu baada ya queen excluder.Box hili huwa ni maalumu kwa nyuki watenda kazi kuweza kuhifadhi asali yao kwa wingi.Asali inayokuwa katika box hili haiwezi kuchanganyika na watoto wa nyuki wala chavua kutokana na kuwapo kwa queen excluder chini yake.Asali inayotoka katika Box hili huwa nzuri na safi kutokana na kutochanganyika na masega ambayo yalitumika kwa kuangulia watoto wa nyuki.
Uvinaji wa asali katika mzinga huu, mfugaji anapaswa kutoa frame zilizopo katika super box ambazo asali yake tayari imeiva.Mara baada ya kutoa frame hizo mfugaji anapaswa kukamua asali hiyo kwa kutumia mashine ya kisasa iitwayo  Honey Centrifuge Machine.Mashine hii huweza kufyonza asali yote iliyopo katika sega na kubakiza sega likiwa halina asali.

Mara baada ya hapo mfugaji anapaswa kurudisha sega hilo kwenye mzinga likiwa na frame yake ili nyuki aweze kujaza asali tena.Hii inamsaidia sana nyuki kumpunguzia kazi ya kujenga sega jipya la Sali kila baada ya mvuno wa asali na hivyo kuongeza uzalishaji wa asali mara dufu.Tofauti tu ya aina ya mzinga huu ni kwamba huwezi kupata zao la nta.

2.      Mzinga wa viunzi
Huu ni mzinga wa teknolojia ya kati kutoka kwenye mizinga ya kienyeji na kuelekea mizinga ya kisasa.Mzinga huu uhifadhi wake wa asali hautofautiani sana na uhifadhi wa asali katika mizinga ya kienyeji, isipokuwa katika mzinga huu masega hupangwa kwa kufuata utaratibu wa viunzi vilivyowekwa.nyuki huweka sega moja katika kila kiunzi kimoja cha mzinga huu.
Mzinga huu pia haujagawanywa kwa kutenganisha sehemu za kuhifadhia asali na sehemu ya malikia kuangulia watoto.Hivyo asali itokayo katika mzinga huu huweza kuchanyanyika na watoto iwapo mfugaji hatakuwa makini katika uvunaji wa asali hiyo.

Uvunaji wa mzinga huu, mfugaji anapaswa kukata sega lote lenye asali pekee na kulihifadhi katika chombo kisafi kwa jili ya kukamua asali hiyo kwa kutumia mashine ya kusasa au kwa kutumia njia za kitamaduni.

PICHA ZA MABANDA TOFAUTI TOFAUTI YA KUFUGIA NYUKI

Picha 1:Banda la kufugia nyuki lililojengwa kwa miti na kuezekwa kwa udongo maarufu kama tembe.
 
Picha 2:Banda la kufugia nyuki lililojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi
 
Picha 3:Nyumba ya kufugia nyuki iliyojengwa kwa matofali na kuwekewa midomo maalumu ya nyuki kwa ajili ya kuingia na kutoka pindi wanapokwenda kutafuta chakula
 
Picha 4:Kibanda kidogo cha kisasa kwa jili ya kufugia nyuki.
Picha 5:Banda la kufugia nyuki lilijengwa kwa miti na kuezekwa kwa bati
 
Picha 6: Banda la kufugia nyuki lilijengwa kwa miti, kuezekwa kwa bati na kuwekewa uzio wa waya.

Share:

TAMBUA TABIA ZA ASILI ZA MAGANJWA YA MIFUGO

UTANGULIZI
Tiba asili kwa karne ya sasa imeonekana kuwa tiba mbadala ya dawa za hospitalini kwa sababu ya madhara yake kuwa madogo kwenye mwili mara baada ya kuyatumia. Madawa haya ya asili yamekuwa yakitumiwa na binadamu tangu enzi hata kabla ya madawa ya kikemikali kuvumbuliwa na mwanadamu. Lakini kasi ya madawa ya kikemikali yalishika kasi kwa sababu ya uharaka wake wa kutibu magonjwa kwa muda mfupi tena kiasi kidogo sana kikitumika. Tatizo la madawa ya asili ilikuwa kutokuwa na uhakika wa dosi na wakati mwingine mgonjwa alihitaji kunywa dawa nyingi sana pasipo mafanikio. Hata hivyo siku za hivi karibuni binadamu ameona ni vema kurejelea dawa za asili huku akifanya maboresho kwa kujua kiasi halisi cha dozi ya dawa. Dawa nyingine zimeboreshwa zaidi na kufanya kiasi kidogo cha dozi kutumika kama dawa za kikemikali tofauti ni madhara machache ya dawa za asili.
Dawa za asili zinahitaji uvumilivu kiasi kwani zinachukua muda ili kufanya kazi huku zikiacha mdhara machache. Dawa hizi zimekuwa zikitumika pia kutibu mifugo hasa kwa zile familia za kifugaji, lakini watu wengine walioibukia ufugaji hawajajua ujuzi huu. Hata hivyo watu mbalimbali wamekuwa wakiandika matumizi ya dawa za asili kwa ajili ya matibabu ya mifugo ili watu wengi zaidi waweze kuzitumia. Hapa chini ni orodha ya miti inayotumika kama dawa kwa ajili ya mifugo na aina ya magonjwa yanayoweza kutibiwa na hiyo miti.

1. SHUBIRI MWITU (ALOE) TIBA YA MAGONJWA YA KUKU 
Shubiri mwitu (Aloe) ni mmea ambao umekuwa ukitumika kwa kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu na mifugo. Mmea huu unatumika sasa kutengeneza sabuni, dawa za binadamu na wanyama na mambo mengine mengi. Na kwa sababu ya madawa mengi ya kiwandani kushindwa kutibu baadhi ya magonjwa kwa sababu wadudu wametengeza ukinzani, ipo haja kubwa ya kuweka umuhimu kwenye madawa ya asili yatokanayo na mimea. Mmea wa aloe vera unauwezo wa kutibu magonjwa ya kuku hasa coccidiosis na kwa kiasi fulani Newcastle disease. Tafiti zilifanyika kwa kutmia mti huu kutibu ugonjwa coccidiosis ambao unamadhara makubwa kwa wafugaji wa kuku zinaonyesha kuwa mti huu unaweza kutumiwa kama mbadala wa dawa za viwandani. 
Maji maji ya mmea huu yanauwezo wa kutibu magonjwa na kuponyesha majeraha yanayotokana na maambukizi ya magonjwa pamoja na kupandisha kinga ya kuku kwa asilimia 50 dhidi ya maonjwa mbalimbali. 
Mmea wa aloe vera unaweza kupandwa maeneo ya karibu na mabanda ya kuku ili kurahisisha upatikanaji wake na unakubali maeneo karibu yote. 
Majina ya mmea huu kulingana na baadhi ya makabila na kimataifa
Jina la Mmea
  • Shubiri mwitu Kiswahili
  • Mkankiruri Kinyaturu
  • Itembwe Kigogo
  • Ibhata Kinyiha
  • Litembwetembwe Kihehe
  • Koli Kikaguru/Kinguu
  • Aloe Kiingereza
  • Aloe vera Kisayansi
Shubiri mwitu kwa ukuaji wa kuku
Kulingana na tafiti zilizofanywa na Bejar (Chuo kikuu cha Kilimo na Misitu cha Samar) na Clapo (Chuo Kikuu cha Ufilipino Mashariki) inaonyesha kuwa ziada ya Shubiri mwitu kwenye maji inasaidia kwa kiasi kikubwa kuku kukua haraka. Mililita 15 had 20 za maji ya shubiri mwitu yakichanganywa na lita tano za maji kila siku kwa kuku 90 yanauwezo wa kusaidia ukuaji wa kuku na kuongeza uzito wa ukilinganisha na wale ambao hawajapewa. 

Uandaaji wa Shubiri mwitu
Kunjwa: Shubiri mwitu (moja) inaweza kukatwe vipande vipande na kulowekwa ndani ya maji ya kunywa kiasi cha lita 1-hadi 3 kutegemeana na idadi ya kuku. Viache humo kwa siku kadhaa hadi unapobadilisha maji ndipo uviweke vingine. Ukiweza kuchuja mchuzi wa shubiri mwitu basi unakuwa ukitumia mililita 15 ndani ya lita tano ya maji ya kunywa kuku kwa kuku 90 kama unakuku wachache basi punguza kiasi cha dawa au ongeza kama ni wengi. 
Vidonda:Kuku wenye vidonda kama kwa ugonjwa wa mdondo (Newcastle Disease) inakubidi utengeneze unga. Kata vipande vidovidogo vya shubiri mwitu kisha changanya na pumba kidogo, vitwange na kuvichekecha ili upate unga laini. Uanike na kisha tunza vizuri tayari kwa kuutumia mara kuku wauguapo. Kuku wenye vidonda waoshwe vizuri kwa maji safi na sabuni pamoja na chumvi kidogo. Baada ya hapo paka unga wa shubiri kwenye vidonda hivyo. 




2. MPAPAI (Carica papaya) DAWA YA KUTIBU MAGONJWA YA MIFUGO
Asili ya mpapai ni Amerika ya Kati. Matunda, majani na utomvu wake hutumiwa kama dawa maeneo mbalimbali ya dunia, matunda na utomvu wake umekuwa ukitumika kutengeneza bombe na waini. Mpapayi una viini hai vingi lakini hivi viwili ni muhimu kwa kutibu magonjwa na kusaidia mmeng’enyo wa chakula ufanyike vizuri: chymopapain and papain. Kiasi cha viini hai hivi hutofautiana kwenye matunda, utomvu, majani na mizizi lakini pia kutegemeana na umri wa mti na njia ya kutengeneza dawa yenyewe.

Matumizi kwa mifugo
  • Kutibu magonjwa ya bakteria: Matawi na mbegu za mpapai vina uwezo wa kutibu magonjwa yanayoenezwa na bakteria hawa: Staphylococcus aureua, Escherichia coli, Salmonella typhi na Bacillus subtilis.
  • Kutibu magonjwa ya fangasi: Utomvu wa mpapai unauwezo wa kutibu fangasi inayoenezwa na Candida albicans
  • Magonjwa ya minyoo:Unga wa mbegu za mpapai unauwezo wa kutibu minyoo ya umbwa inayojulikana kama Dirofilaria immitis (inayoshambulia moyo). Wapewe dozi ya milligram 60 kwa kila kilo moja ya uzito wa mbwa kwa muda wa siku 30. Minyoo mingine pia inaweza kutibiwa na mmea wa mpapai kama Ascaris suum kwa nguruwe katika dozi kati ya milligram 4-8 kwa kila kilo moja ya uzito wa nguruwe kwa muda wa siku 7. Utibuji wa minyoo kwa mifugo ndiyo kivutiuo kwa wafugaji.
  • Mpapai pia unauwezo wa kusaidia mnyama aharishe ili kutoa kitu ambacho hakifai tumboni.




Kwa binadamu mmea huu umekuwa ukitumika sehemu mbalimbali kutibu magonjwa/matatizo yafuatayo: Kuharisha na kuharisha damu, magonjwa ya figo, ini, kichaa, mafua, homa, kuongeza utoaji wa maziwa, matatizo ya mmeng’enyo wa chakula, vidonda na asthma.
Share:

FAHAMU JINSI YA KULIMA UYOGA NA FAIDA ZAKE KATIKA MWILI WA MWANADAMU

FAHAMU JINSI YA KULIMA UYOGA NA FAIDA ZAKE KATIKA MWILI WA MWANADAMU


 
UTANGULIZI.
 
Uyoga ni aina ya nyuzi kuvu (fungus) yenye kutofautiana na mimea mingine kwa kukosa chembe chembe zinazowezesha mimea kujitengenezea chakula yenyewe kwa kutumia hewa na mwanga.
Uyoga unaota wenyewe kwenye mashamba hasa wakati wa mvua kwenye maeneo yenye mboji nyingi. Sasa hivi nchini tunao utaalamu wa kuotesha uyoga au ndani ya nyumba au nje kwenye kivuli maalumu.

 
HISTORIA FUPI YA UYOGA.
Uyoga umefahamika na wanadamu tangu enzi za zamani sana. Miaka elfu nne kabla ya kuzaliwa Kristo watu walijua uyoga. Historia inatueleza kwamba watu wameanza kulima kwa utaalamu mwaka 300 baada ya kuzaliwa Kristo.
Wadadisi wa mambo wanauelezea Uyoga kufanana sana na chakula waisraeli walichokuwa wakila kule jangwani katika safari yao ya kutoka utumwani Misri.
Wakati Uyoga ukilimwa katika dunia yote, hapa Afrika na hasa kwetu Tanzania mambo yalikuwa ni tofauti kabisa. Hakuna mtu aliyesumbuka na kilimo hicho. Ni hapo majuzi tu mwaka 1993 ndipo ukulima ulianza Dar es salaam. Mwaka 1994 ukulima ulianza Arusha, mwaka 1995 ukulima ulianza huko Mbeya, na mwaka 2003 ukulima ulianza huko Kilimanjaro.

 
AINA YA UYOGA.

 
Inakadiriwa kuwa kuna aina milioni moja na laki tano (1,500,000) za nyuzi kuvu (fungus) duniani; katika hizi ni aina 64,000 ambazo zimekwisha kufanyiwa utafiti na kupatiwa maelezo ya kisayansi. Katika hizi aina 64,000, kuna ambazo zimethibitika kuwa na Uyoga halali 12,000. Na kati ya hizi ni aina 2,000 na ndizo zinazolimwa.
Katika aina 2,000 za uyoga zilizokwisha thtbitika, hapa Tanzania ni aina 40 tu.
Uyoga Mamama (Oyster mushroom).
Aina hii ya Uyoga hustawi katika nchi za Tropics. Utaalamu unaohitajika siyo mgumu. Baadhi ya aina zinazooteshwa ni hizi zifuatazo;
. Pleurotus oystreotus
. Pleaurotus sajo-caju
. Pleaurotus sapidus
. Pleurotus flabel atus - (pink oyster)
. Leaurotus Pulmonerius
. H. K. n.k
. Monkey Head
. Auriclaria
Nyingine zinazooteshwa hapa nchini kwa kiasi kidogo ni;
. Agaricus bitoquis (uyoga vifungu)
Uyoga taka ambazo ni;
. Coprinus cinereus
. Caprinus Comatus
. Lentinus edodes
. Volvoriella Volvocea
Nyingine ni;
. Ganodema lucidum

 FAIDA ZA UYOGA
Uyoga una maajabu makubwa katika maisha ya mwanadamu, Uyoga ni lishe bora kwa mwanadamu, ni dawa na tiba kwa mwanadamu, ni zao la kuingizia watu kipato, ni rafiki wa mazingira pia.
LISHE
. Uyoga ni zao lenye viini lishe (amino acids) zote 22 zinazohitajika na mwili wa mwanadamu.
. Protini iliyoko kwenye Uyoga inafikia kiwango cha asilimia arobaini. Hii inalingana na protini iliyoko kwenye maziwa.
. Kuna wingi mkubwa sana wa vitamini B,C na D.
. Uyoga hauna mafuta mengi. Una asilimia tatu tu. Hivyo hauna Colestrol.
. Uyoga unayo madini yote muhimu kwa mwanadamu; phosphorus, Iron, Calcium na Potash.
TIBA
Utafiti uliofanyika siku za karibuni umethibitisha kuwepo kwa dawa nyingi ndani ya uyoga zenye uwezo wa kutibu kwa ufanisi, magonjwa ya wanadamu na mifugo. Kwa wanadamu magonjwa yafuatayo yanatibiwa;
. Kifua kikuu TB
. HIV/AID upungufu wa kinga mwilini
. Kisukari
. Shinikizo la damu
. Magonjwa ya moyo na uti wa mgongo
. Saratani
. Matatizo ya figo
. Vifo vya watoto wachanga
AJIRA
Kwa sasa hivi ajira imepungua sana katika nchi yetu. Vijana, wazee na rika lote hatuna kazi, mazao yaliyokuwa yakituingizia kipato yamepungua au yamekwisha. Nguvu kazi nyingi tuliyonayo inatumika kuuza mwanasesere na plastic zinazotoka katika nchi za nje.
Watu wengi mno tunaishi katika lindi la ufukara. Hatuna mahitaji ya msingi kama vile chakula, malazi na mavazi bora. Kufuatana na ripoti ya umoja wa mataifa, iliyoandaliwa na Professors S. T. Chang na Mshigeni wa chuo kikuu cha Namibia, mauzo ya Kahawa kwenye soko la ulimwengu kwa mwaka 1997 ni dola za kimarekani bilioni 15. Mauzo ya Uyoga yalikuwa dola bilioni 14. Katika biashara hiyo Afrika ilichangia kwa asilimia 0.3 tu.
Wataalamu hawa wanaainisha sababu nyingi zinazosababisha upungufu huu. Kubwa wanalosema ni kuwa waafrika hawajui umihimu wa uyoga katika maisha ya mwanadamu. Bei ya uyoga huko Marekani, Mashariki ya kati na Mashariki ya Mbali ni kati ya dola za Marekani tisa ($9) hadi kumi na tatu ($13). Uyoga ni zao lililo kayika mpango nafuu wa biashara ya Marekani na Afrika. Halitozwi ushuru kuingia katika masoko ya Marekani.


 
KUSAFISHA MAZINGIRA
Kufuatana na ripoti ya wataalamu wa chuo kikuu Kivais na Magingo ya miaka ya tisini, Tanzania inayo masalio ya kilimo na misitu zaidi ya tani milioni kumi na saba (17,000,000). Masalio haya yameachwa yakioza, au kuchomwa moto au kulishwa mchwa pamoja na mapanya. Ikiwa masalio haya yatatumika kuoteshea Uyoga, Mazingira yataboreka na uchumi utakua. Uzalishaji wa Uyoga unaanzia pale mkulima au mtumiaji wa bidhaa za kilimo na misitu anapomalizia.

 
MASALIO YA TAKATAKA BAADA YA KUOTESHA UYOGA.
Masalio ya takataka (vimeng'enywe) hutumika kama ifuatavyo;
. KULISHA MIFUGO
Uyoga una uwezo wa kuvunja vunja chembe chembe za vimeng'enywe na kuviboresha kuwa protini na madini mengi, kisha kufyonza hicho na kutengeneza matunda ya uyoga. Baada ya kuvuna uyoga chembechembe hizi bado zina ubora mkubwa wa chakula kwa ajili ya mifugo kama vile ng'ombe, mbuzi, nguruwe, sungura n.k. Tunao wafugaji wanaotumia vimeng'enywe hivi kulishia mifugo nao wameendelea kupata maziwa mengi.
. MBOLEA
Vimeng'enywe hivi hutumika kama mbolea shambani na katika bustani. Matokeo ya kutumia vimeng'enywe hivi yameonyesha ufanisi mkubwa.
.METHANE GAS
Tukijenga mfumo wa kutengeneza gesi kama kawaida, tunaweza kutumia vimeng'enywe hivi kutengeneza methane gas. Hii gesi itatumika kupikia, kuwasha taa na mambo mengine kama hayo. Mabaki katika zoezi hili huwa na mbolea nzuri ifaayo sana. Mazao ya shamba na bustani yaliyokuzwa kwa mbolea hii yana bei nzuri zaidi sokoni, maana yanahesabika yamezalishwa kiasili (organic agriculture).
. ZERI ( Zero Emmission Research Initiative).
Umoja wa Mataiga umeiteua Tanzania pamoja na nchi nyingine katika bara la Afrika kuendeleza na kutekeleza mfumo wa ZERI. Huu ni mfumo wa kutochafua mazingira kwa njia ya kutoa moshi. Masalia ya kilimo ba misitu yasichomwe moto bali yageuzwe kutoka hali yake na kuwa kitu kingine labda kilicho bora na chenye thamani zaidi. Masalia ya sokoni hatutayaacha yaoze bure, tutayasindika ili yaweze kuzalishia uyoga. Pumba za mpunga na kahawa hatutazichoma moto. Tutazitumia kwa kuzitengenezea chipboards, vivyo hivyo na maranda ya mbao, takataka za katani, kahawa na n.k. zitageuzwa kuwa kitu bora zaidi.
 
UTAYARISHAJI WA SHAMBA LA UYOGA.
Mambo ya muhimu ya kuzingatia:
. Ukubwa wa shamba
. Uwezekano wa upanuzi
. Usafi wa eneo
. Upatikanaji wa takataka za kulimia yaani vimeng'enywe 
. Upatikanaji wa maji safi
. Umbali kutoka kwenye soko
Ndani ya ndani
. Hewa safi ya inayozunguka
. Joto linalotakiwa
. Unyevunyevu kwenye hewa unaotakiwa
. Carbondioxide na mwanga vinatakiwa
Shamba
Shamba la uyoga linapaswa liwe na viambatanisho vifuatavyo;
. Sehemu ya kutayarisha vimeng'enywe
. Kichanja cha kuhifadhi majani au aina yoyote nyingine ya vimeng'enywe.
. Sehemu ya kuchemshia vimeng'enywe

. Sehemu ya kupandia mbegu kwenye vimeng'enywe vilivyokwisha kuchemshwa.
. Banda kamili la kukuzia lenye sifa zilizokwisha ainishwa hapo juu
. Sehemu ya kuhifadhia uyoga uliovunwa au chumba cha baridi kutegemea na hali halisi.

 
UJENZI WA SHAMBA
Mkulima anashauriwa kutumia vifaa vinavyopatikana katika eneo lenyewe. Kwa mfano mkulima mwenye shamba la migomba, baai atumie marawa katika kuta na paa. Unaweza ukatumia nyasi za kawaida au majani ya mpunga, ngano na mengine ya namna hiyo, unaweza kutumia matofali mabichi, unaweza kutumia mabanzi. Ndani ya nyumba weka weupe. Hii ni chokaa au kitambaa cheupe. Hii ni kwa sababu uyoga hukua kuelekea rangi ya mazingira yaliyouzunguka. Lakini rangi nyeupe huchochea ukuaji na hudumisha usafi. Nyumba ya uyoga iwe na madirisha makubwa mazuri.

 
MAANDALIZI YA VIMENG'ENYWE
Kama ilivyosemwa hapo mwanzo, kila jani lililokomaa na kukauka, lafaa kuoteshea uyoga. Michanganyiko ifuatayo yafaa sana kuoteshea uyoga.
. Majani ya mpunga au migomba yenye unyevu 62%
. Pumba za mahindi unyevu 62%
. Sukari
. Chokaa
Vimeng'enywe viko vingi, mkulima anashauriwa awaone wataalamu kwa ushauri.
MAHITAJI MENGINE
Ifuatayo ni orodha ya mahitaji mengine;
. Jiko la kuchemshia
. Pipa tupu la lita mia mbili
. Mifuko ya plastic size 10" × 15" yenye uwezo wa kuhimili joto
. Viroba (polysacks) pvs ya kuweka ndani ya pipa
. Vibangili vya kipenyo cha 1.5
. Kamba au uzi wa kushonea viatu ili kufunga mifuko wakati wa kuchemsha.
. Vipande vya magazeti
. Rubber band size ya mpira wa ndana ya tairi ya baiskeli.

 
HATUA ZA KUFUATA KATIKA KUOTESHA
. Katakata majani yaliyokomaa na makavu katika urefu usiozidi nchi nne
. Changanya majani haya na virutubisho hapo juu i.e. pumba za mahindi, sukari na chokaa.
. Changanya sawasawa kwa kutumia maji safi ndoo tatu hadi tano.
. Zilundike mahali safi ukitengeneza mlinduko wenye kimo cha mita moja hadi mita moja na nusu.
. Funika kwa polythene paper na vitambaa vya sulphate 
. Majani ya migomba yalowekwe kwa siku mbili hadi tatu kabla ya kuvundikwa
. Ziache kwa muda wa masaa 24
. Weka vimeng'enywe hivi katika mifuko ya polythene
. Weka maji lita 40 katika pipa lenye kichanja cha mbao chenye kuzuia mifuko isigusane na maji
. Bandika kwenye jiko hadi mvuke unapotoka , hesabu msaa manne.
. Ipua mifuko yako na iweke mahali safi
. Sasa ni wakati wa kufanya kila kitu kwa hali usafi. Tunatumia maji yenye detol kusuzia mikono yetu
. Otesha uyoga kama mtaalamu atakavyokuonyesha
. Baada ya siku 21 ondoa vipande vya gazeti ulivyotumia kufunika mifuko
. Baada ya siku 10 nyingine utaanza kuvuna uyoga. Uta una kwa muda wa miezi 2 hadi 3
. Weka uyoga uliovuna ili kuhifadhi ubora wa uyoga.
MAPATO YA MKULIMA
Tunaorodhesha hapa hali halisi ya mkulima wetu mwenye banda la mita tatu (3) kwa mita tano (5).
Gharama:
Majani ya mpunga Pickup moja = 25,000/-
Mifuko ya plastic 500@50 = 25,000/-
Mbegu za uyoga chupa 100@1500 = 150,000/-
Jumla = 200,000/-

Mavuno aliyopata kilo 300@3000 = 900,000/-
Toa gharama = 200,000/-
Salio = 700,000/-
Kazi hii ilimchukua mkulima huyu miezi mitatu. Ijulikane kuwa baada ya kuotesha mkulima anakagua banda kw muda mfupi sana, asubuhi saa sita na jioni. Mkulima huyu na familia yake anajipatia wastani wa shilingi 230,000/- kila mwezi kwa kulima banda moja.
MAPISHI
Mkulima na umma wote wanapashwa kujua mapishi ya uyoga. 
Tunaweza kutumia uyoga kama ifuatavyo;
. Kutengeneza supu
. Kutengeneza supu ya viungo (mushroom curry) 
. Kutengeneza mboga ya kawaida tunayoweza kula na vyakula vingine kama vile ugali ndizi, wali, viazi n.k.
. Tunaweza kuzindika a kutengeneza mushroom pickle (hii tutauza kwenye supermarket na mahoteli ya kawaida hasa ya kitalii)
. Tunaweza kutengeneza mushroom pizza.

 
MAGONJWA YA UYOGA
Uyoga ni viumbe hai. Hivyo hupatwa na magonjwa kama hali ya mazingira na utendaji haitakidhi. Kuna magonjwa ya aina kama ifutavyo;
. Bacteria
Uyoga unakuwa na rangi ya kutu. Hata mifuniko inakuwa na rangi hiyo. Ugonjwa huu unatambulika kiurahisi., kwani unakuwa unateleza.
. Fungus
Aina zifuatazo ndizo hasa zishajulikana;
. Blue mould
. Black mould
. Brown mould
. Virus
Uyoga uliopendeza unasinyaa mara moja. Unaanza kutoka jasho.

 
MASOKO
Mpaka sasa hoteli za kitalii zinapika uyoga wa kutoka nje uliowekwa kwenye makopo. 
Ikumbukwe kuwa kwenye makopo kuna uyoga halisi kidogo sana. Pia katika supermarket za hapa nchini kuna uyoga fresh kutoka Kenya. Pia tujue kuwa majirani wetu waliotuzunguka Kenya, Uganda, Zambia na Malawi wamepiga hatua kubwa katika kilimo cha uyoga. Swali tunalopaswa tujiulize sote ni hili " Kulikoni Tanzania kuhusu Uyoga".
Tumeziona faida za uyoga. Ni bora kuliko nyama nyekundu na nyama nyeupe. Kwenye maduka ya nyama zinauzwa kilo nyingi za nyama kila siku. Badala yake tuuze uyoga kila siku.

 
SOKO LA NJE
Kama ilivyoelekezwa hapo juu kuna masoko ya nje. Lakini yanataka kiasi kikubwa cha uyoga. Tani kadhaa kila wiki na kila mwezi. Ili kuweza kukidhi haja hii, wakulima waunde vikundi na vyama vya ushirika ili kushughurikia jambo hili.

 
HITIMISHO
Andiko hili dogo lina lengo la kumuandaa Mtanzania wa kawaida aweze kuwa mkulima wa uyoga. Kamwe lisichukuliwe kama mamlaka tosha kuhusu uyoga. Sababu ni kwamba nimechagua kuzungumzia yale mepesi tu yanayoweza kumfaa mkulima wa ngazi ya mwanzo. Sayansi ya uyoga ni pana, ndefu na yenye kina.
Ahsanteni sana.
Imeandaliwa na kuandikwa na Marcodenis E. Misungwi,
Mtaalamu wa Kilimo na Mifugo III, Mbozi District Council
Kwa msaada wa International Fund for Agricultural Development, IFAD
Share:

DRONE CAMERA KWA BIE POWA

tomtop.com INT

PHONES

tomtop.com INT

.

https://ad.admitad.com/shuffle/45eb471090/

.

Total Pageviews

PATA SIMU NZURI KUTOKA NJE

Aliexpress INT

Labels