HII NDIO NJIA RAHISI AMBAYO UNAWEZA KUITUMIA KUZALISHA KUKU CHOTARA
Leo tutaangalia kuhusu ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa kutumia njia rahisi. Na jinsi gani unaweza kuzalisha kuku chotara. Kuku chotara ni mchanganyiko wa kuku wa kienyeji na kisasa. Kabla hatujangalia hatua muhimu za kuzalisha kuku chotara, tutaangalia faida za kuku chotara kwa mwekezaji/mjasiriamali.
Faida za kuku chotara kwa mfugaji na mlaji
Ukuaji mzuri
Nyama yake ina ladha nzuri na laini
Nyama yake ina ladha nzuri na laini
n.k
Hawa ni kati ya kuku chotara ambao ninafuga
HATUA MUHIMU KATIKA UZALISHAJI WA KUKU CHOTARA
Hatua ya kwanza, andaa banda lako ambalo linafaa kwa matumizi ya ufugaji wa kuku, banda la kuku linatakiwa liwe lina pitisha hewa ya kutosha na kama unataka kufahamu kwa undani kuhusu maandalizi muhimu ya banda lako. Makala hiyo itakuja kupitia blog yako ya uwekezaji na mtanzania.
Hatua ya pil,i andaa kuku wa kienyeji matetea (majike) na jogoo la kisasa aina ya kocks au aina yoyote ile ambayo inafaa, wachanganye kuku wa kienyeji na jogoo la kisasa katika banda moja ili uweze kupata mayayi yenye mchanganyiko wa kuku wa kienyeji na kisasa. Kumbuka jogoo mmoja (1)anatakiwa kuwa na matetea kumi na tano (15) au matetea yasizidi kumi na tano.
Hatua ya tatu kutotolesha mayayi ambayo umeyapata kutokana na mchanganyiko wako, unaweza kutumia mashine za kutotolesha mayayi au unaweza kuwatumia matetea yako ya kuku wa kienyeji kuatamia mayayi yako.
Hatua ya nne baada ya siku ishirini na moja (21), vifaranga vyako vitakuwa tayari kwa kutumia matetea ya kuku wa kienyeji au mashine ya kutotolesha vifaranga kwa ajilia ya matunzo mpaka wakiwa wakubwa. Vifaranga vikishakuwa tayari chanjo muhimu wanahitaji ili kuzuia vifo na mripuko wa magonjwa. Vifaranga kwa muda wa wiki tatu hadi nne wanahitaji joto la kutosha, kwa ajili ya ukuaji afya njema.
Chanjo na dawa muhimu kwa vifaranga mpaka wakiwa wakubwa
Siku 2-6 Pullorum Trisulmycine,Trimazine 30%au Cotrim+Vitalyte,Amin’total au Broiler booster maji
Siku ya 7 Mdondo(newcastle) Newcastle vaccine(Lasota maji
Siku 14 Gumboro Gumboro (Bursine vaccine-IBD) maji
Siku 16-20 Coccidiosis Trisulmycine/Trimazine/Esb3 30%+Dawa yoyote ya Vitamin maji
Siku 21 mdondo(newcastle) Newcastle vaccine(Lasota) maji
Siku 28 Gumboro Gumboro (Bursine vaccine-IBD) maji
Wiki ya 6-8 Ndui Fowl pox vaccine sindano kwenye bawa
Wiki ya 13 minyoo Pipperazine cirtrate+Dawa yoyote ya vitamin maji
Wiki ya 10 hadi ya 15 ukataji midomo Dawa ya vitamin itumike baada ya zoezi maji

KUMBUKA
Dawa ya minyoo na chanjo ya kideli kila baada ya miezi mitatu
0 comments:
Post a Comment