HII NDIO BIASHARA UNAYOWEZA FANYA KWA MTAJI MDOGO NA KUTENGENZA PESA?
HII NDIO BIASHARA UNAYOWEZA FANYA KWA MTAJI MDOGO NA KUTENGENZA PESA?
Tatizo la ajira limeendea kuwa kikwazo kikubwa cha wahitimu wengi wanaomaliza masomo yao katika ngazi mbalimbali hapa nchini na hata kwa wale ambao hakufanikiwa kuendelea na masomo. Huku sekta ambayo inatoa ajira nyingi kwa wahitimu ni sekta binafsi. JE WE KIJANA UNAKUBALIANA NA TATIZO LA KUKOSA AJIRA HUKU UKISUBIRI SERIKALI?
Suluhisho la tatizo lako liko hapa ndugu, unaweza kujiari kwa mtaji mdogo na ukatengeneza pesa. Nadhani utajiuliza ni biashara gani au ni shughli ipi ambayo inaweza kukuingizia kipato kwa mtaji mdogo. KILIMO CHA UYOGA kati ya biashara ambayo hazihitaji mtaji mkubwa, ni kilimo ambacho hakihitaji mtaji mkubwa sana, kwa wewe kijana ambaye una lengo la kutengeneza pesa hili ni kati ya suluhisho linalokufaha. Bei ya kilo ya Uyoga ni kuanzia Shilingi 6,000 mpaka 12,000 kwa kilo, bei zina tofautia kutokana na maeneo
HISTORIA FUPI KUHUSU KILIMO CHA UYOGA HAPA TANZANIA
Miaka ya karibuni, utaalamu wa kuotesha uyoga umeanza hapa Tanzania baada ya watu kutilia maanani lishe bora ya protini na manufaa mengine ya zao hilo. Kwa kuwa uyoga upo wa aina mbalimbali, usitawishaji wake hutofautiana katika mahitaji yake, ikiwa ni pamoja na hali ya hewa, malighafi za kuoteshea, urahisi wa teknologia ya kuotesha katika mazingira ya Tanzania na soko lake kwa wananchi na katika hotel. Hata hivyo ni wananchi wachache tu wanaojua kilimo cha uyoga.
MAHITAJI KATIKA KILIMO CHA UYOGA
Mbegu za uyoga huzalishwa kwenye maabara zenye vifaa vinavyowezesha kuotesha mbegu hizo bila kuchafuliwa au kuchanganyika na vimelea kama bakteria, ukungu au jamii nyingine za uyoga ambazo haziliwi.
Hapa Tanzania hivi sasa maabara hizo zipo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kituo cha utafiti wa kilimo-Uyole na taasisi ya utafiti wa kilimo cha bustani- Tengeru (HORTI – Tengeru, Arusha). Hata kwenye maduka ya kilimo na mifugo.
Mahitaji mengine
1. Pipa
2. Majani ya migomba
3. Maranda
4. Visado au lailoni
Somo hili la kilimo cha uyoga litakuja wiki ijayo kupitia blog yako UWEKEZAJI NA MTANZINIA
0 comments:
Post a Comment